Swahili
Surah Ash-Shams ( The Sun ) - Aya count 15
وَالشَّمْسِ وَضُحَاهَا
( 1 ) ![Swahili - Ash-Shams ( The Sun ) - Aya 1 Ash-Shams ( The Sun ) - Aya 1](style/islamic/icons/mp3.png)
Naapa kwa jua na mwangaza wake!
وَالْقَمَرِ إِذَا تَلَاهَا
( 2 ) ![Swahili - Ash-Shams ( The Sun ) - Aya 2 Ash-Shams ( The Sun ) - Aya 2](style/islamic/icons/mp3.png)
Na kwa mwezi unapo lifuatia!
وَالنَّهَارِ إِذَا جَلَّاهَا
( 3 ) ![Swahili - Ash-Shams ( The Sun ) - Aya 3 Ash-Shams ( The Sun ) - Aya 3](style/islamic/icons/mp3.png)
Na kwa mchana unapo lidhihirisha!
وَاللَّيْلِ إِذَا يَغْشَاهَا
( 4 ) ![Swahili - Ash-Shams ( The Sun ) - Aya 4 Ash-Shams ( The Sun ) - Aya 4](style/islamic/icons/mp3.png)
Na kwa usiku unapo lifunika!
وَالسَّمَاءِ وَمَا بَنَاهَا
( 5 ) ![Swahili - Ash-Shams ( The Sun ) - Aya 5 Ash-Shams ( The Sun ) - Aya 5](style/islamic/icons/mp3.png)
Na kwa mbingu na kwa aliye ijenga!
وَالْأَرْضِ وَمَا طَحَاهَا
( 6 ) ![Swahili - Ash-Shams ( The Sun ) - Aya 6 Ash-Shams ( The Sun ) - Aya 6](style/islamic/icons/mp3.png)
Na kwa ardhi na kwa aliye itandaza!
وَنَفْسٍ وَمَا سَوَّاهَا
( 7 ) ![Swahili - Ash-Shams ( The Sun ) - Aya 7 Ash-Shams ( The Sun ) - Aya 7](style/islamic/icons/mp3.png)
Na kwa nafsi na kwa aliye itengeneza!
فَأَلْهَمَهَا فُجُورَهَا وَتَقْوَاهَا
( 8 ) ![Swahili - Ash-Shams ( The Sun ) - Aya 8 Ash-Shams ( The Sun ) - Aya 8](style/islamic/icons/mp3.png)
Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake,
قَدْ أَفْلَحَ مَن زَكَّاهَا
( 9 ) ![Swahili - Ash-Shams ( The Sun ) - Aya 9 Ash-Shams ( The Sun ) - Aya 9](style/islamic/icons/mp3.png)
Hakika amefanikiwa aliye itakasa,
وَقَدْ خَابَ مَن دَسَّاهَا
( 10 ) ![Swahili - Ash-Shams ( The Sun ) - Aya 10 Ash-Shams ( The Sun ) - Aya 10](style/islamic/icons/mp3.png)
Na hakika amekhasiri aliye iviza.
كَذَّبَتْ ثَمُودُ بِطَغْوَاهَا
( 11 ) ![Swahili - Ash-Shams ( The Sun ) - Aya 11 Ash-Shams ( The Sun ) - Aya 11](style/islamic/icons/mp3.png)
Kina Thamudi walikadhibisha kwa sababu ya upotofu wao,
إِذِ انبَعَثَ أَشْقَاهَا
( 12 ) ![Swahili - Ash-Shams ( The Sun ) - Aya 12 Ash-Shams ( The Sun ) - Aya 12](style/islamic/icons/mp3.png)
Alipo simama mwovu wao mkubwa,
فَقَالَ لَهُمْ رَسُولُ اللَّهِ نَاقَةَ اللَّهِ وَسُقْيَاهَا
( 13 ) ![Swahili - Ash-Shams ( The Sun ) - Aya 13 Ash-Shams ( The Sun ) - Aya 13](style/islamic/icons/mp3.png)
Hapo Mtume wa Mwenyezi Mungu alipo waambia: Huyu ni ngamia wa Mwenyezi Mungu, mwacheni anywe maji fungu lake.
فَكَذَّبُوهُ فَعَقَرُوهَا فَدَمْدَمَ عَلَيْهِمْ رَبُّهُم بِذَنبِهِمْ فَسَوَّاهَا
( 14 ) ![Swahili - Ash-Shams ( The Sun ) - Aya 14 Ash-Shams ( The Sun ) - Aya 14](style/islamic/icons/mp3.png)
Lakini walimkadhibisha na wakamchinja ngamia, kwa hivyo Mola wao Mlezi aliwaangamiza kwa sababu ya dhambi zao na akawafuta kabisa.
وَلَا يَخَافُ عُقْبَاهَا
( 15 ) ![Swahili - Ash-Shams ( The Sun ) - Aya 15 Ash-Shams ( The Sun ) - Aya 15](style/islamic/icons/mp3.png)
Wala Yeye haogopi matokeo yake.